Kaa La Moto aingia Bongo movie
Hivi majuzi tu Kaa La Moto alikua nchi jirani ya tanzania ambapo alishirikishwa katika movie. Katika movie hio, Kaa ameigiza kama mwanawe muigizaji mkongwe wa bongo movie, Mhogo Mchungu na Bi Rehema.
Vilevile Kaa akiwa ni mmoja wa wasanii wanaokuza kiswahili, akiwa Tanzania, Kaa alipata fursa mya kuwekwa katika orodha ya wasanii watakaofanya kazi na BAKITA (Baraza la Kiswahili Tanzania), baraza lenye mipango ya kukuza kiswahili kupitia sanaa Africa Mashariki.
Comments
Post a Comment