Kauli ya Mchekeshaji Kingwendu baada ya Kukosa kupata ubunge wa jimbo la Kisarawe


Muigizaji na mchekeshaji Kingwendu aliyekua anagombania kiti cha ubunge jimbo la Kisarawe alikua mmoja ya mastaa wa bongo waliokua wanapigania vyeo mbali mbali katika uchaguzi mkuu uliofanyika siku ya Jumapili 25, Octoba 2015. Mastaa wengine waliokua wakigombania nyadhfa mbalimbali ni kama vile mwigizaji Frank, Professor Jay na Afande Sele.

Baada ya kutofanikiwa kunyakua kiti hicho cha ubunge, alikua na haya ya kusema:
Kiukweli kabisa matokeo ya mwanzo kabisa ilikua inaonyesha mimi naongoza lakini baada ya kumaliza kuhesabu kura ikaonekana amenishinda yule bwana Suleiman Jafo wa CCM...Nimejaribu na nimethubutu kwa mara ya kwanza kugombea nafasi kubwa ya Ubunge.. nimeenda vizuri tu na sitachoka na wala sitaacha, najipanga tena kwa mara nyingine najua nimekosea wapi na ntajipanga upya na ntaenda kusomea siasa zaidi..

Mwaka 2020 huko nadhani nitakua niko sawa, nakwenda kusomea siasa zaidi ili niijue siasa zaidi na nijue nitamkamata wapi, kuhusu kushawishiwa kuingia kwenye siasa, hakuna mtu aliyenishawishi kugombea ubunge bali ni mimi mwenyewe niliamua baada ya kuona pia baadhi ya wasanii wenzangu wanagombania kama nilivyomuona Mr. II Sugu kipindi kile.

Comments

Popular posts from this blog

ThrowBackTrack.... MACHUNGU - Daddy Sele