Jamaa ajinyakulia dola 500 katika shindano la mwanamme mwenye sura mbaya zaidi


Kuna mashindano mengi duniani, kama vile ya urembo, mvuto, kupendeza ila pia usishangae kwa hili kwani pia nchini Zimbabwe kuna mashindano ya mtu mwenye sura mbaya zaidi.
Maison Sere, ambaye hana meno kadhaa mdomoni aliwapiku washindani wengine watano na kukwarua mkwanja mrefu kiulaaiiiiiini. Jombi huyu mwenye umri wa miaka 42 aliyeibuka mshindi katika shindano hili la kua na sura mbaya zaidi  hana kibarua alituzwa kitita cha dola 500 kwa kua na sura mbaya zaidi.

Kama kawaida, katika kila shindano, hakukosi malalamiko haswa washindani wasiokubali kushinwa na shindano hili pia lilipata malalmiko kutoka kwa mshindani William Masvinu ambaye amewahi kushinda shindano hilo mara tatu mtawalia alilalamika na kusema kwamba mshindi Miason alipendelewa ndiposa yeye akaibuka wapili lakini yeye ndiye aliyestahili tuzo hio.

Shindani hilo limegonga vichwa vya habari na hii hapa ripoti kutoka kwa kitua cha CCTV, China
 

Comments

Popular posts from this blog

ThrowBackTrack.... MACHUNGU - Daddy Sele