KideKide yateuliwa katika Tuzo za Pulse Music Video Awards
Kilicho na sifa kipewe sifa na kazi nzuri siku zote haifichiki kwani kwa kila kila njia hua itajiuza tu. KideKide ya Dazlah aliyomshirikisha Susumila ni track ambayo imetamba sana katika anga za mziki na kwa takriban miezi saba saa hii, ndiyo wimbo kutoka pwani unaoongoza kwa kuchezwa sana.
Hit hii ambayo ilitayarishwa na Producer Tee wa Tee Hits na video ya wimbo huu ambayoo ndio imeteuliwa iliongozwa na kutayarishwa na Hamza Omar wa ONE MONTAGE FILMS imeweza kuteuliwa katika tuzo za PULSE MUSIC VIDEO AWARDS katika kitengo cha BREAKTHROUGH VIDEO OF THE YEAR.
Katika tuzo hizo zenye vitengo 10, KideKide ndio wimbo wa pekee kutoka pwani.Ushindi wa Dazlah na Susumila na sanaa ya pwani kwa ujumla iko mikononi mwako kwani mshindi anabainiwa kwa wingi wa kura zitakazopigwa na mashabiki.Tuwe wazalendo na kwa pamoja tuweze kuwapa Dazla na Susumila uwezo wa kunyakua tuzo hii kwa kutuma ujumbe mfupi wa neno PMWA8a na utume kwa 22845, KWA GARAMA YA SHILINGI MOJA TU. Vilevile unaweza kupiga kura online kupitia LINK HII(bonyeza hapa)
Comments
Post a Comment