Mtangazaji wa Baraka F.M,Nelly Mwikamba apata pigo
Hapo jana, mtangazaji wa Baraka F.M ambaye amewahi kushinda tuzo mbili Nelly Mwikamba alipata pigo. Mume wa Nelly Mwikamba alihusika katika ajali mbaya ya barabara wakati akiendesha gari. Bwanake Nelly aligonga gari nyeupe aina ya Harrier maeneo ya Shanzu katika barabara kuu ya Mombasa-Malindi. Katika ajali hio, alivunjika mfupa wa paja mara mbili na anatarajiwa kufanyiwa upasuaji baadae hii leo.Upasuaji huo unatarajiwa kugharimu takribani shilingi Laki Tano.
Nelly ambaye ni hivi majuzi tu alijaaliwa mtoto huendesha kipindi cha jioni kwa jina ON THE LANE akishirikiana na Captain Lui. Pia ni mmoja wa walioteuliwa kuwania Mtangazaji Bora wa Kike katika tuzo za Nzumari zitakazofanyika tarehe 11 mwezi wa Disemba katika hoteli ya kifahari ya Flamingo Beach
-kutoka kwa meza yetu ya habari tunamtaki bwanake Nelly afueni ya haraka
Comments
Post a Comment