Producer Amz aondoka SQ Records


Producer wa hits kama vile Tuliza Nyavu, Chanda Chema, My Voice My Choice, Producer Amz ametangaza kutoka rasmi katika studio za SQ. Ikiwa hii leo ndio ambayo Amz anakamilisha miaka mitano kuhudumu kama producer wa SQ Records, ndio siku ambayo AMZ amejitoa rasmi katika studio hio.
Sq Records ilifunguliwa mwaka wa 2008 na ma,producer waliotangulia kufanya kazi SQ ni V-Sita, TK2, Shirko na Kroniqs. Hio inamaana Amz ndiye producer aliyedumu kwa mda mrefu ndani ya SQ Records.

Kupitia kwa njia ya simu Amz ameeleza ya kwamba ameamua kutoka SQ na anajipanga kuja na stuio yake kwa jina TEMPOZ ambaye itaanza kazi rasmi Januari 2016.
Vipi kuhusu kazi alizokua anazishuhulikia?
"kwa sasa kazi hizo hazipo, Steve (mmiliki wa SQ Records) alianiambia ya kwamba harddisk ziliibiwa wakati studio ilipokua inafanyiwa ukarabati".... AMZ alieleza

Comments

Post a Comment

Popular posts from this blog

ThrowBackTrack.... MACHUNGU - Daddy Sele