Susumila na Kush Tracey kurudia Video ya wimbo UMENITOSHA



Video ya msanii SUSUMILA akimshirikisha mwanadada  KUSH TRACEY ni moja kati ya zile projects ambazo zimesubiriwa sana na mashabiki wengi  wa mziki kwa sasa. Ukizingatia kuwa ni moja kati ya kazi ambazo zilipigiwa debe sana huku picha za utayarishaji wake zikitawala mitandaoni. Ni dhahiri kwamba subira ya wengi imefikia kikomo na uvumilivu wa wengi umeanza kutibuka.


Kwa wengi walio na maswali kuhusu video ya wimbo huu wanafaa kujua kuanzia leo kuwa baadhi ya vipande vya video hiyo havikutokea ilivyotakikana kwa hivyo video hiyo inapangwa kurudiwa tena ili kurekebisha makosa yaliyokuwepo. 

Mbali na video ya umenitosha,  msanii SUSUMILA alikua ameahidi ngoma kadhaa ikiwemo video ya wimbo aliyoshirikishwa na  Dazlah, Bangereba Rmx.

Tukisubiriavideo rasmi ya wimbo huo, kunayo video yake ya animation iliyotayarishwa na Rikky Bekko ikiwa ndio video ya kwanza ya mtindo wa animation kuwahi kufanyiwa msanii wa Pwani.

Comments

Popular posts from this blog

ThrowBackTrack.... MACHUNGU - Daddy Sele