Familia ya mwanamziki wa Injili, Annastacia Mukabwa yanusurika katika ajali
Ni msimu wa Krismasi na watu wengi wako katika pilkapilka za kusafiri ili kujiunga na familia zao katika kusherehekea skukuu ya Krismasi.
Asubui ya leo, midaa ya saa moja katika maeneo ya Makindu, familia ya muimbaji wa Injili, Annastacia Mukabwa imenusurika kutoka kwa ajili mbaya ya barabarani. Wakiwa wanaelekea kijijijini ambako tayari Annastacia alikua ametangulia, Mume, watoto na dereva wa gari yao binafsi walipatwa na mkosi huo.
Nikiongea naye kwa njia ya simu, Annastacia alieleza ya kwamba tairi la gari lilipasuka hivyo basi kusababaisha dereva kushindwa kudhibiti gari hilo, katika ile hali ya kuepuka kugonga gari zingine barabarani, dereva amejikakamua kuelekeza gari kando ya barabara, lakini alipokanyaga brake ndipo gari lilipo bingiria mara tatu.
Gari limeharibika vibaya lakini kwa bahati nzuri wote waliokuwemo katika gari hilo wamenusurika na majeraha madogo tu.
Comments
Post a Comment