Kampeni ya #PlayMyMusic ya Ng'oa Nanga hapa MOMBASA
SANITA NZARO, mwanzilishi wa tuzo za Pwani Celebrity Awards akishirikiana na Wizara ya Vijana, Jinsia na Michezo, Mombasa County ameanzisha kampeni ya #PlayMyMusic. Kampeni hii ni ya kupigania na kuhakikisha ya kwamba asilimia 60 ya mziki unaochezwa katika maeneno ya burudani ni mziki kutoka Mombasa. Hii ni kujaribu kuwezesha wasanii waweze kupata kipato kupitia royalties na wasanii kupata exposure vizuri kwa mashabik.
Kampeni hio ambayo ilianzishwa rasmi na waziri wa vijana, jinsia na michezo Mheshimiwa Mohammed Abbas hapo jana katika Pwani Showcase Night iliyofanyika Bliss Resort. Akiongea katika uzinduzi huo, Mheshimiwa Abbas alisema kwamba hivi karibuni sana, watakua na mkutano na wamiliki wa maeneo ya burudani ili kupanga mikakati hio itakayowezesha lengo la kampeni hio kufanikishwa. Vilevile, aliahidi ya kwamba kutakuwepo na sheria katika kaunti ya Mombasa kusisitiza na kuhimizia ya kwamba mziki unaochezwa katika maeneo ya burudani iwe asilimia 60.
Sanita alieleza ya kwamba ni vigumu sana kuandaa show ya msanii/wasanii wa Mombasa ukapata crowd kama inavyopaswa kwa sababu mashabiki wanashabikia sana wasanii wa nje, na si kwa sababu hawawapeni wasanii wa Mombasa lakini ni kwasababu mziki unaofikishwa kwa mashabiki na ma,dj kutoka kwa wasanii wa Mombasa ni kidogo sana, hivyo basi kufanya wasanii wa mombasa kukosa kupenya vizuri katika soko la hapa nyumbani.
Sanita pia amesifu sana vituo vya redio hapa Mombasa , Pwani kwa ujumla kwani wanajitahidi sana kucheza mziki wa nyumbani na kuwapa fursa wasanii wanaochipuka. Ombi kubwa kwa Sanita ni support kutoka kwa wasanii na anawaomba wasanii watumia hashtag #PlayMyMusic kuonyesha support na ku,create awareness.
Wiki hii kutakua na misururu ya mikutano uitakayohusishwa washikadau wa Kampeni hio na habari za yatakayojiri utayapata hapahapa na kupitia ukurasa wa Sanita Nzaro,
Comments
Post a Comment