Kundi jipya kutoka Mkubwa Na Wanawe
Mkubwa Fella, ambaye ndiye mmiliki wa kituo cha talanta cha Mkubwa na Wanawe ambako ndio walikotokea Yamoto Band amezindua kundi lingine tena la vijana saba amabo ndani yao ni binti mmoja.
Vijana wenyewe ni OSAMA, PODO, STARBOY, ZUBERI, STAR MAPOZI, ABUUADO na FETTY.
Kulingana na Fella, kundi hilo kwa jina SALAMU TMK ni vijana anaowatoa mtaani na wanahitaji kufika mjini na kupata nguvu binafsi ya kujikimu.
Kundi hili jipya tayari lina video mpya iliyoongozwa na Pablo ya wimbo mpya kwa jina NAFSI.
Comments
Post a Comment