Barnaba kwenye Collabo nyengine tena na wasanii wa Mombasa
Ni mmoja kati ya wasanii wakongwe wa mziki wa kizazi kipya. Amekua aki,hit kila uchao si kwao nyumbani Tanzania tu, bali Afrika Mashariki kwa Ujumla. Naongea kuhusu hitmaker wa Milele Daima, Elias Barnaba almaaruf Barnaba Boy aka Barnaba Classic.
Hivi majuzi alshirikishwa na mwanadada kutoka hapahapa nyumbani, Sis P katika remix ya wimbo wa Bonge La Bwana. Siku za majuzi Lamini3, ambalo ni kundi la wasanii kutoka hapa Mombasa linaloundwa na SingleJay, Chriss na Sauda, walifika Tanzania kutayarisha mziki kwa Producer mtajika Bongo-C9.
Wakati wakiwa studio wakirecord, Barnaba aliwaskia na akawasifu sana. Vijana hawakuzubaa kwani hapohapo walimuomba Barnaba aingie katika track hio na bila kusita Barnaba aka,record part yake.
Kwa hivi sasa Lamini3 wanaendelea kutayarisha video hio ya wimbo DANCE ambao wanatarajia kuachia wakati wowote mwezi wa Februari utakapoanza. Kando na DANCE, kuna track pia Lamini3 wamemshirikisha Nay wa Mitego
Comments
Post a Comment