FOUR MOST INFLUENTIAL YOUTHS IN MOMBASA
ALI KUBO
Mzaliwa huyu wa Mombasa ambaye alisoma katika shule ya Sekondari ya Tononoka na Chuo cha Ufundi
cha Mombasa( T.U.M) ni mmoja kati ya vijana walio na ushawishi mwingi
katika kaunti ya Mombasa. Kubo ni mpigapicha, mwanamitindo, mwanahabari na pia
muigizaji. Kubo amewahi kushiriki katika kipindi cha Mombasati na pia video za muziki kadhaa kama vile
Kitete, ya Amoury, Barua ya Rais- SudiBoy/Jaguar, Dogo Richie na kwa sasa
anashirikishwa kuandaa movie kwa jina MOYO nchini Tanzania.
Kubo ana ukaribu sana na wanasiasa wengi, kama vile mbunge
wa Mvita, Abdulswamad, Gavana Joho na Seneta Sarai. Ukaribu wake na wanasiasa
hawa umemfanya kutumika kufanya kazi na vijana na wanasiasa hawa, hivyo basi
kuweza kumfanya kuwa na ushawishi mkubwa katika
jamii. Ukaribu huo na wanasiasa umezua minong’ono ya kwamba Kubo
anaandaliwa kupigania moja ya viti vya visiasa… kama ni kweli, ni kiti gani
atapigania na katika eneo gani? Ni 2017 au 2022?
ANITA NZARO
Ni kielelezo kizuri cha kwamba pale mtu anapotia bidii basi
hua amefunga pingu za maisha na mafanikio.
Anita alianza kama kijakazi Saudia pindi tu baada ya kumaliza
shule. Baada ya kurudi kutoka Saudia, alifungua biashara ya salon na vilevile
kua mwanamitindo na kushiriki katika video za mziki. Baadae aliandikwa kazi ya kufuta majani na
kampuni ya Ketepa Tea. Hio ni kabla ya kuanzisha kampuni yake ya
Ashantyz Promotions ambayo ilimsaidia kuwa project manager katika ofisi ya naibu gavana wa kaunti ya
Kilifi.
Anita ambaye pia ndio mwanzilishi wa Pwani Celebrity Awards mwanzoni
mwa mwaka aliweza kuteuliwa kuwa co-host katika kipindi cha Mseto EA ambacho ni
moja kati ya vipindi vya mziki/burudani vinavyotazamwa sana hapa nchini. Ukizingatia ya
kwamba ameekeza katika tasnia ya
burudani ambayo ndio inayohusisha vijana wengi, imempa ukaribu pia na wanasiasa katika kaunti ya
Mombasa kama vile Waziri wa wizara ya vijana, jinsia na michezo ya kaunti ya
Mombasa, Mohammed Abbas na naibu wa Gavana wa kaunti ya Kilifi ambao
wote wanajishuhulisha sana na projects za vijana.
ALFRED MWAKIO
Alfred ambaye anaelekea miaka 30, ni mzaaliwa wa Changamwe(Chaani) kwa
sasa ni naibu waziri katika wizara ya
vijana, jinsia na michezo baada ya kuhamishwa kutoka wizara ya Usafiri katika
kaunti ya Mombasa. Alfred ambaye ana shahada ya Economics & Management
kutoka chuo cha Belgorod State Technology University, Moscow pia alisomea I.T
katika chuo cha Institute of Advanced Technology , Afrika Kusini na pia
Vororezh Institute Of High Technology, Moscow.
Kabla kuajiriwa na kaunti ya Mombasa, Alfred alikua mfundi wa mambo ya Uchumi katika kampunitatu-Sethman Marine, Baba Shipping na Geo Wave Contractors.
Kufanya kazi katika kaunti haswa
wizara ya vijana kumemuweka karibu na wanasiasa kama vile
Seneta wa Nairobi Mike Sonko, Gavana
Joho, Seneta Sarai, waziri Mohammed Abbas. Alfred alikua kiongozi wa wanafunzi
kutoka Afrika alipokua chuoni Moscow. Pia ni mwanzilishi wa #WordToTheYouth movement. Vile vile ni m,wakilishi wa ONUG (One Nation Under God) na pia Amani Pwani. Ukaribu wake na wanasiasa
na kujihusisha na projects za vijana kumeashiria ya kwamba huenda akawa
anajitayarishwa kuingia katika ulingo wa siasa. Kama ni kweli, ni 2017 au 2022?
SUSUMILA
Ni
mmoja kati ya wasanii wakongwe na ambao wanawafuasi wengi si Mombasa Tu, bali Pwani kwa ujumla. Toka
aanze mziki 2007 Susumila amekua akitoa hit baada ya hit kila ucho. Ukiangalia
safari yake ya mziki amefanya mitindo mingi ya mziki, kama vile Hiphop,
Raggaton, Chakacha, Nduara na Afrobeat. Wepesi wake wa kubadilisha mtindo na
wakati ndio umemsaidia yeye kua na mashabiki wengi wa kila aina na ukizingatia ya
kua hajawahi oumzika basi imemfanya yeye kuwa mwenye ramani ya mziki kwa mda
mrefu sana.Susumila kuwa na mashabaiki wengi kumempa ushawishi mkubwa kwani ametumika kufanya matangazo ya biashara na siasa kwa mfano wimbo wake wa Ngangari ambao aliubadilisha kumpigia debe Gavana Hassan Joho wakati wa uchaguzi. Kuna fununu ya kwamba Susumila huenda akajirusha katika siasa katika Kaunti ya Kilifi katika uchaguzi ujao.
Comments
Post a Comment