JE KAA LA MOTO ANA SIFA ZA KUITWA LEGEND WA HIP HOP?


Hivi ni inawezekana msanii aka,hit bila kutoa wimbo mpaka akajulikana kila kona ya mtaa? Katika hali ya ushindani iliyopo kwa sasa katika tasnia ya mziki ni wazi kwamba endapo yupo mtu anayeweza kufanya hivyo basi tuko na kila sababu kumpa sifa zote kwani ni dhahiri kuwa kwake sifa zitakua zimefika nyumbani. Endapo utakua umefuatilia kwa makini nyendo na safari ya msanii wa hip hop KAA LA MOTO tangu alipokua anachipuka hadi sasa utagundua kwamba watu walimjua kwanza kupitia uwezo wake wa kuchana kwenye rap battles cyphers pamoja na kualikwa katika vipindi mbalimbali vya redio mfano MASHAV MASHAV ya Gates Mgenge ambako kila alipokwenda alitema nyongo kiasi kwamba watu mtaani walimkubali tu kupitia ubora wake wa ku freestyle na uwezo wake wa kuheshimu nguzo zote za hip hop kupitia ubunifu wa hali ya juu na punchlines. 

Hadi sasa ukichunguza zaidi ijapokua msanii huyu ametoa nyimbo nyingi saana zenye mafunzo na zenye uzito wa mashairi ukweli ni kwamba hazijahit kulingana na umaarufu wake ulivyo mkubwa afrika mashariki. Hii inaonyesha wazi kwamba mbali na track anazotoa kuna misingi mingi pamoja na kanuni zinazomuongoza na kumfanya ajizolee mashabiki kila kukicha. Juhudi zake za kuwa msanii tofauti zimemfanya kujizolea tuzo kubwa za pwani pamoja na kuvikwa taji la kuwa miongoni mwa wasanii kidogo bora wa hip hop Kenya nzima wenye ufanisi wa mitindo huru na punchlines nahii inadhihirika wazi baada ya kutajwa kama atakayewakilisha pwani kwenye tamasha la who is king litakalofanyika tarehe 30 jijini Nairobi. 
Ni tamasha lenye hadhi kubwa kwani kaa la moto atakua anajiunga na wasanii wakubwa kutoka Nairobi kama vile Khaligraph Jones, Rabbit, Juliani pamoja na majina mengine makubwa ya hip hop humu nnchini. Kupitia mziki wa HipHop, Kaa La Moto amefanikiwa kujipata kwenye runinga pekee ya pwani, Pwani TV kama mtangazaji wa kipindi cha HIPHOP TEKETEKE kila siku ya alhamisi. 

Harakati za msanii huyu zimesaidia sana kubadili mtazamo wa watu wengi kuhusu mziki wa hip hop kuwa ni uhuni na kujenga taswira mpya ya mziki huu kupendwa na kila rika na labda kwa wale wasiojua ni kwamba KLM ni mmoja kati ya wale wasanii wa HIP HOP wasiotumia uraibu wowote wa pombe wala madawa ya kulevya. Kulingana na Kaa La Moto mwenyewe ni kwamba kufikia sasa anaweza asitoe wimbo kwa kipindi cha mda mrefu na bado akazidi kupeta kwa sababu uwezo wake alionao wa punchlines na freestyle umemjengea brand ambayo imempa heshima kubwa saana east afrika.

Kwa mtazamo wangu mimi binafsi ni kwamba huu ni mfumo mgumu saana kwa msanii kuutumia na kufanikiwa na endapo mtu atafanikiwa kuutumia basi mtu huyo ana kila kigezo na sababu ya kuitwa LEGEND AU MWALIMU MKUU KWENYE DARASA LA HIP HOP… Huyu hapa KAA LA MOTO msikilize akizungumzia show ya who is the king itakayofanyika Nairobi mwisho wa mwezi ambayo yeye amechaguliwa kuiwakilisha pwani.
BONYEZA HAPA KUMSKILIZA KAA LA MOTO 

Comments

  1. Kaa la moto nampa pongezi, kweli anayo nguvu ya kufika mbadi na anadiserve kuitwa LEGEND AU MWALIMU MKUU KWENYE DARASA LA HIP HOP. Kila la heri bro Kaa La Motto....

    ReplyDelete
    Replies
    1. anajua mafans wake wanataka nini anajua kubadilika na wakati

      Delete

Post a Comment

Popular posts from this blog

ThrowBackTrack.... MACHUNGU - Daddy Sele