Wema atarajia kujifungua mtoto wa Idris Sultan mwezi wa Agosti
Mshindi wa Big Brother Africa, Idris Sultan alidhibitisha ule uvumi uliokuwepo katika mitandao ya kwamba Wema ana ujauzito na yeye ndio jimbi. Kupitia account yake, Idris alithibitisha ya kwamba Wema ni mama kijacho na anafuraha sana kwa kua yeye ndio mhusika wa kiumbe kijacho na anajivunia mabadiliko na furaha Wema aliyoleta katika maisha yake.
Baaade, katika mahojiano na Clouds FM, Idris alifunguka na kusema ya kwamba wanatarajia mtoto wao baada ya miezi 6 au 7 hivi. Idris alitiririka zaidi na kusema ya kwamba yeye binafsi anapenda sana ajue jinsia ya mwanawe kabla kuzaliwa kwani hataki aanze matayarisho ya kumpokea mtoto anunue vigauni kumbe mtoto ni wa kiume, lakini mzazi mwenzake, Wema anampiga kwa hilo kwani anataka jinsia ya mwanawao iwe surprise.
Akimalizia alieleza ya kwamba, karibuni watafunga pingu za maisha na hawezi kuzuia watu kuongea kwa kua mara sometimes watu hua wagumu kupokea mabadiliko lakini anaamini masiku yanavyosonga watu wataelewa tu.
Comments
Post a Comment