Artiste To Watch This year
Hassan Salim ndio jina lake halisi lakini katika sanaa anajulikana kama Kelechi Africana. Ni chipukizi ambaye aliachia wimbo wake wa kwanza huu mwaka lakini ameshangaza wengi kwa uwezo wake mkubwa alio nao kiasi ya kwamba ukimuita chiopukizi ni kama wamuonea vile.Ana style unique ya mziki ambayo yeye mwenyewe anaiita AfriNAIJA, styl ambayo anachanganya kizungu, kiswahili, kimijikenda na mahadhi ya kinaijeria.
Aliachia wimbo wake wa kwanza kwa jina Bomboribo mwishoni mwa Januari na baadae aliashirikishwa katika wimbo For Me wa Alyento. Kwakua ana bidii ya kazi na meneja wake ambaye ni Athman Babaz ameamua Africana ni kazi tu mwenda mbele na mwaka ni track tu baada ya track,mwezi huu wa Februari, Kelechi akishirikiana na Wasojali Band waliachia wimbo kwa jina Nitalia Nawe ambao umetokea kupendwa sana na unapeta sana katika chati za mziki hapa pwani.
Nitalia Nawe ndio project ambayo ataifungulia mwezi wa March kwani ndio video yake itakapokua inadondoshwa na mwezi huohuo ataachia audio na video ya track nyingine kwa jina NO WAY.
"Tunavyoongea nipo studio na Producer Noizer tukimalizia kuandaa track yangu ya Tano ambayo nidhani nitaiita Ndere na Inshallah nitaiachia mwezi wa April iwapo hakuna chochcote kitakacho badilika kulingana na mipango yetu"...Kelechi alinielezea kwa njia ya simu.
bonyeza hapa kuskiliza BOMBORIBO
bonyeza hapa kuskiliza NITALIA NAWE
bonyeza hapa kuskiliza FOR ME
Comments
Post a Comment