Barua Kwa ma,Presenter na ma,DJ kwa niaba ya Wasanii
Juzi niliandika barua kwa wasanii kwa niaba ya Presenter na Dj, Leo nachukua fursa hii kuwakabidhi barua ma,presenter na ma,DJ kwa niaba ya wasanii maana mtaani kuna lawama kibaoo.......
Naelewa kuwa katika barua niliyoandika juzi nilisema kuwa kuchezwa kwenye redio sio haki ya msingi kwa msanii, ila hii haimaanishi kuwa napigia debe uozo ambao umeletwa na watangazaji na ma,Dj ambao kwa kiwango kikubwa sana wana nafasi kubwa sana katika tasnia ya mziki. Kwa kiwango kikubwa sana kifo cha mziki wa hapa nyumbani kinasababishwa na hawa wadau wawili DJ na PRESENTER.
Hivi ni picha gani unayoipata Presenter anaijua historia yooote ya msanii Kanye West ila hatambui hata wasanii wawili wa nyumbani wanaotrend mtaani? Top ten chat ya radio station iko Mombasa imetawaliwa na nyimbo za Nigeria na marekani. Hivi inamaanisha nyumbani hakuna wasanii? Wasanii wengi wamelalamika kwamba katika baadhi ya vipindi wanalazimishwa kuhonga ndio nyimbo zao zichezwe hewani. Hivi ina maana kuwa hawa kina Davido na kina Drake pia huwa wanahonga au ndio ile ile nidhamu ya ukoloni mambo leo wa kubabaikia vya nje ndio tujivike "ustaarabu" feki ambao unapanda mbegu ya umaskini kwa sanaa ya nyumbani
.
Sikatai kuna mziki mwingi wa nyumbani ambao hauna vigezo vya kufikia kiwango cha kuchezwa redioni ila kuna asilimia kubwa saana ya mziki mzuri wa nyumbani ambao kwa sasa uko sokoni wenye vigezo vya hali ya juu kutoshea katika ratiba ya vipindi vya kila kituo cha redio. Ila kufikia sasa mazoea yameiondoa kabisa heshima ya msanii wa nyumbani kufikia kiwango cha kuwa msanii wa nje anapewa heshima kubwa sana na faida inayopatikana kutokana na support wanayopewa wasanii hao wa nje haionekani. Imefikia kiwango sasa wasanii wamelazimika kubadilisha mfumo wengine wanalazimisha kuimba kiingereza au ki Nigeria angalau tu wapate nafasi kwenye playlist za radio hali ambayo imeathiri ubora na uhalisia wa sanaa yetu.
Presenter kuweka mziki usio vigezo hewani kisa amelipwa hela ni moja kati ya virusi vikali vinavyoua sanaa ya nyumbani maana katika hali hii tunatengeneza mazingira ya mwenye hela mpishe na sio mwenye kipaji. Ila sio rahisi kupata Dj au Presenter mwenye ameitambua hatari hii.
Tasnia ya mziki wa nyumbani haiwezi tanua iwapo mziki mzuri utakandamizwa kisa msanii hana pesa za kuhonga, vile vile mziki wa nyumbani kamwe hauwezi kufikia levels za juu kama washikadau wakuu kama Dj na Presenter watakubali kuukuza mziki wa nje na kuupuzilia vipaji vya nyumbani. Hakuna kitu cha kusikitisha kama msanii wa nyumbani mwenye kipaji wimbo wake uchezwe mara moja kwa mwezi wakati wimbo wa sijui kina Davido na kina Drake unatawala kwenye playlists kila siku. Maendeleo ya sanaa yetu kwa sasa yanahitaji maandamano makubwa saana ya kifikra na kila mshika dau awajibikie jukumu lake.
Ma DJ na PRESENTERS wengi wana unafiki wa kumtafuta msanii baada ya kuwa amekubalika ila kama bado chipukizi anaonekana kimeo tu.
Alafu hapo ndio mnalaumu msanii akiwaonyesha shobo anapofanikiwa kwa juhudi zake mwenyewe mkisahau kwamba dunia duara. LETS SUPPORT OUR OWN, tusibabaikie watu ambao hawatutambui. Japo msanii hana haki ya msingi ya kuchezwa kwenye redio fikiria kwamba ukiutangaza mziki wa nyumbani msanii akipanua soko na kufanya show basi haukuzi kipaji tu bali pia unabuni na kuimarisha uchumi.
....itakayofuata ni barua kutoka kwa presenter kwenda kwa producer
Kweli kabisa..mimi Ni msanii na Nina masikitiko makubwa Sana kuona kwamba hatupewi nafasi kamwe..mpaka uhongane ndio wimbo uchezwe..na hats ukihongana unachezwa kidogo Tu hadi uongeze hela zingine tena na tena....nimechoka!!!
ReplyDelete