Barua Kwa Wasanii Kwa Niaba Ya Mapresenter Na Ma,DJ
Kama hadi sasa wewe ni msanii ambaye kila ukishuka unaelekeza lawama kwa Presenter au DJ nahisi ya kwamba itakua vizuri sana kama ungewacha mziki taratiiiiiibu na ujitaftie shuhli nyingine ufanye.
Huu ni mtazamo wangu binafsi ila nahisi ni mtazamo ambao hata bila kupitishwa na mtu yoyote utakua una chembe chembe za ukweli ndani yake. Mimi binafsi huenda ikawa sijui changamoto wanazopitia wasanii ila kwa kiwango kikubwa saana nazielewa sana changamoto wanazozipitia haswa watangazaji.
Kwanza kabisa ukianza kulalamika kuhusu presenter flani kutocheza mziki wako jiulize kwanza presenter huyo kwa siku hupokea ngoma ngapi kwa e mail yake, pili jiulize je mziki wako una hadhi ya kutosha kuhimili ushindani uliopo, tatu je mziki wako una viwango vya kumletea faida na kumuongezea soko yule presenter au DJ katika kazi yake?
Ukishajiuliza maswali yote haya nahisi kwamba utapata jibu kwamba msanii na Presenter au DJ wanafaa kuwa na ushirikiano mkubwa sana ambao unafaa kuwa wa kikazi na sio kishkaji. Nishawahi kusema na hua nasema mara nyingi sana ya kwamba, katika harakati za kutaka mziki wako utawale airwaves kwa sasa lazma uendane na wakati na pia uwe na ubunifu wa hali ya juu sana ili utoe kazi zenye viwango vitakavyokidhi mahitaji ya soko.
Wewe kama msanii unapopeleka kazi kwa Presenter akupe support ukae ukijua kwamba yule Presenter au yule DJ pia yuko mbioni kuimarisha ubora wa kipindi chake au biashara yake hivyo basi hana Lawama kabisa anapokanyagia mziki usioendana na viwango vyake. DJ yuko pale kibiashara Presenter yuko pale kikazi kaandikwa hivyo basi hawezi kuhatarisha soko lake kwa kigezo cha kumridhisha msanii ambaye hayuko serious.
Kauli yangu ya mwisho ni kwamba: wewe kama msanii, toa kazi nzuri, wakikataa kuzicheza kwa redio, plartforms ziko nyingi sana za kuufikisha mziki wako kwa mashabiki wako. Siku hizi mitandao imejaa, blog zipo tu sana kwa kazi hizo. Vituo vya redio sio vyombo vya umma kwamba utakua na haki ya msingi mziki wako uchezwe. Msanii piga kazi safi mwisho watakutafuta wenyewe Lakini ukiendelea kutojiamini mbele ya ma,Presenter, mwisho wa siku UTAPIGA DEKI NYUMBANI KWAO ILIMRADI TU UCHEZWE KWE REDIO.
Comments
Post a Comment