DJ Kaytrixx Ajitosa Katika Siasa


Uchaguzi unakaribia na watu wengi wa taaluma mbali mbali wameonyesha ari ya kuwania viti mbalimbali katika uchaguzi mwakani. Washikadau katika tasnia ya burudani pia hawajawachwa nyuma, kwani hapa pwani Cannibal na Mtaliano Eliano ni miongoni wa wasanii waliotangaza nia zao za kugombaia viti vya MCA. CEO wa Spin Cycle Entertainment Limited, DJ Kaytrix naye hajawachwa nyuma.
Nyota yake ilianza kung'aa katika kinyang'anyiro cha “Pilsner Mfalme” mwaka wa 2008 wakati alipowakilishwa Pwani na kuebuka numba 5. Januari 2009 alijiunga na CodeRed kwa mda wa miaka miwili kabla kuanza kuwa binafsi mnamo 2011 na kuanzisha Dj Unit yake ya Spin Cycle Entertainment Limited ambayo ime,sign dj kama vile  Mr T, Xclusive, Bonez, Phauz na Scream.
Kaytrixx ambaye amewahi kufanya show nyingi nchini Rwanda na Tanzania vilevile alitangaza ya kwamba anapania kuwania kiti cha MCA katika ward ya Mikindani katika uchaguzi wa 2017. Akitangaza maamuzi hayo, Kaytrixx alihimiza watu wajisajili ili wakati wa uchaguzi wawe na uwezo wa kuchagua viongozi wanaowaridhisha na sera zao zitaleta manufaa katika jamii.

Comments

  1. N sawa kwa uamuzi Wao kwani naona pia vijana wanaamka...all the best #kichwa_kibovu...#eliano_mtaliano...na #DJ ktrix

    ReplyDelete

Post a Comment

Popular posts from this blog

ThrowBackTrack.... MACHUNGU - Daddy Sele