Kidis ajibu madai ya Kuzalisha mschana na kumtelekeza
Baada ya mschana kwa jina Agnes kujitokeza na kusema ya kwamba muimbaji wa Viroboto alimpachika mimba na kumtelekeza yeye na mwamawe wa kike ambaye kwa sasa ana mwezi mmoja Kidis amefunguka kuhusu madai hayo.
Kidis ambaye kwa sasa yuko nchini Tanzania, hapo Ijumaa alihojiwa na Gates Mgenge katika kipindi cha MashavMashav, Pwani FM kwa njia ya simu, alisema ya kwamba kama kuna yeyote ambaye ana uhakika ya kwamba ana mtoto wake basi amplekee kwani yeye hawezi kukataa damu yake.
Gates alimuuliza iwapo anamjua Agnes na jibu la Kidis ilikua ya kwamba hamjui Agness lakini iwapo ana mtoto wake na ana uhakika ni wake ampelekee kwa kua hawezi kataa damu yake.
Comments
Post a Comment