Susumila Aongelea Kuhusu Ndoa, Track 3 ambazo zilimuinua sana mwaka jana na mambo mengi kumhusu

Susumila alifunguka na kusema ya kwamba kando na kufanya track 12 mwaka jana, kuna track 3 ambazo zilimpa mafanikio makubwa sana kwenye mziki. Susumila alikiri ya kwamba yeye kujaaliwa mke mwema mwaka jana ndio ilikua achievement kubwa sana mwaka jana, alisema ya kwamba Ihale, Tuliza Nyavu na KideKide ndio track ambazo zilimuinua sana katika sanaa ya mziki mwaka jana.

Kuhusu mapokezi kwa mashabiki wake mwaka huu, Susumila ameweka wazi shukrani zake kwa mapokezi mazuri ya track kali aliyofanya na msanii wa nairobi KAKA SUNGURA inayokwenda kwa jina la mapepe. Kulingana na Susumila, mapokezi mazuri ya track hiyo haswa katika miji ya Mombasa na Nairobi yanampa kila sababu ya kuamini kuwa mwaka huu tayari umeanza vizuri kwa upande wake. Susumila amesema kuwa kwa sasa tayari yeye na msanii mwenzake kaka sungura wako mbioni kuandaa utayarishaji wa video ya wimbo wa Mapepe ambayo wanapania ku shoot tarehe 10 mwezi ujao jijini Nairobi.

Msanii huyu ambaye aliandikisha mafanikio makubwa katika safari yake ya mziki mwaka jana amefunguka na kusema kwamba kuwa tangu aingie kwenye ndoa safari yake ya mziki imechukua mfumo mpya ambao amedinda kuuweka wazi. Kuhusu swala hilo hilo la ndoa, Susumila amepuuzilia mbali dhana iliyopo kwamba msanii akioa hushuka kimuziki huku akihoji kuwa wako wasanii wengi ambao hawajaoa na wameshuka kimuziki.

Comments

Popular posts from this blog

ThrowBackTrack.... MACHUNGU - Daddy Sele