Unamjua Sis Shanniez? Je ushawahi kumuona akiwa kazini? hii hapa ni fursa yakipekee ya kukujuza
Anaitwa Sis Shanniez aka Anti Virus, majina aliobatizwa katika mwezi wake wa kwanza alipofanya kipindi kutokana na misimamo yake mikali kuhusu tasnia ya mziki kanda ya pwani.Ni mtangazaji wa kipindi cha Kaya Flavaz, kila siku jumatatu hadi ijumaa kuanzia saa tatu asubuhi kipindi ambacho kinapeperushwa katika Radio Kaya- 93.1 fm msa, 99.7 fm mlnd, 94.9fm voi, kituo ambacho makao yake makuu yako mjini Kwale.
Amekua kwenye tasnia ya utangazaji kwa mda wa miaka 5. Anajulikana sana kwa kuwa presenter mwenye msimamo asiyeyumbishwa kirahisi na kuwa na msimamo thabithi katika vitu anavyotaka kufanya.
Jambo ambalo wengi hawajui kuhusu Sis Shanniez, dada ambaye ana mapenzi mengi na sanaa ya hapa pwani na anajifua sana kuona ya kwamba sanaa ya mziki hapa nyumbani inaendelea ni kwamba ana dada mmoja tu mdogo ambaye anampenda sana. Wengi wamekiri ya kwamba wanatamani sana kumuona Shanniez akiwa kazi, na kama shukrani kwa mashabiki wake wanaomuunga mkono kazi yake na kumpa motisha hii hapa ni zawadi aliyoitoa angalau wamuone akiwa kazini... Tazama...
Comments
Post a Comment