Chidi Benz Anahitaji Msaada
Msanii mkongwe wa hiphop, Rashidi Abdallah Makwiro aka Chidi Benz amejitokeza na kusema ya kwamba hayuko sawa kwa sasa na anahitaji msaada.
Chidi Benz ambaye wengi wamekua wakisema anatumia madawa ya kulevya, madai ambayo yalitiliwa mkazo pale aliponaswa na madawa ya kulevya aina ya heroine na bangi mwaka 2014. Mwaka huo huo Dully Sykes akijaribu kumsaidia Chidi arudi kwenye game alimkutanisha na AY na Diamond wakafanya ngoma-MPAKA KUCHE. Diamond alikiri ya kwamba Chidi Benz alimsaidia kutoka kwa aimuomba collabo alipokua chini na Chidi Benz hakumuonyesha nyodo na wakafanya "Nalia na Mengi" bila kumuitisha hata sumni. Lakini ni kama msaada huyo haukudumu kwa mda mrefu.
Tusonge mbele kidogo... mwishoni mwa wiki jana, Chidi Benz akihojiwa katika Clouds TV alishtua wengi kwani jinsi alivyokonda si mchezo.Chidi alisema ya kwamba uwezo wa mziki bado anao ila wale wadai wanaoshikilia mziki wamemtupa.Chidi alisema ya kwamba angekua kwenye game kwa sasa wana hiphop wengi wasingekuwepo kwani angewafunika ndio maana hajasaidiwa kwa kua wengi hawataki awepo kwani angewatoa ake na Joh Makini na wengineo.
Chidi alisema ya kwamba ijapokua afya yake imezorota, hivi majuzi alipiga show kwa masaa mawili kitu ambacho kilimfanya mamake kulia na kumwambia ya kwamba ameona jinsi mwanawe alivyofanya show kali na watu wanavyomshabikia lakini haoni mwamko wa watu kumsaidia, heri wafanya mpango watu wamsaidie.
Chidi Benz alisema anataka asaidiwe, anatamani kusaidiwa kwani pia yeye anatamani mafanikio kama aliyonayo Diamond.
Okay hii hali yake mbaya sana..mbona kakondeleana hivi ..kudadadeki!
ReplyDelete