DJ Lenium Apata Bonge La Dili
Ni moja ya malengo ya kila mtu maarufu haswaa katika tasnia ya burudani kuweza kutumia brand au jina lake kupitia jina lake kupata pesa. Mkongwe katika tasnia ya burudani hapa Mombasa, jamaa ambaye anajivunia kuwa katika industry kwa miaka kumi na pia kuwa na tuzo kumi, kiasi cha tuzo ambacho hakuna yeyote hapa mkoani awewahi kufikisha, Daktari Wa Mziki aka Dj Lenium wiki hii alipata bonge la shavu.
Wiki hii, kampuni ya teksi ya Uber ilipokua ikitangaza kuanzisha huduma zake Mombasa, pia ilizindua mabalozi wake wawili, ikiwa ni Dj Lenium na Miss Tourism, Tima Keilah. Nilimtafta DJ Lenium angalau anidokezee kama alilambishwa mkwanja wa kiasi gani lakini akadinda kufunguka kiundani na kujibu kwa kicheko akisema "nimelishwa vizuri boss"
Comments
Post a Comment