Dogo Richie Atambulisha Label Yake Na Msanii Wake Wa Kwanza

Dogo Richie ambaye kwa sasa anafanya vizuri saana na wimbo wake wa yoyobah amesema kwamba lengo la kuanzisha label hiyo ni kushughulikia msukukumo ambao amekua akiupata kutoka kwa wasanii wenye vipai wanaohitaji msaada wa kutambulishwa sokoni. Kupitia usemi wake label hiyo ilianza kama group ya whatssap na mwishowe wakafikia katika kiwango cha kumsaidia mmoja wa member wa group hiyo kwa kuwa alionyesha uwezo wa hali ya juu wa vocals. Dogo Richie amesema kuwa kwa sasa wameanza na msanii mmoja kwa jina SHYMAN ambaye wanapania kumpa support ya kutosha hadi atoke.
ShyMan ni jamaa maarufu hapa mkoani haswaa kwa wasikilizaji wa vipindi  vya mziki wa Afrika Mashariki katika redioza hapa mkoani kwani hua ni vigumu sana kipindi kuisha vila kumskiza amepiga simu redioni. Ni shabiki sugu sa wa mziki wa pwani na mimi binafsi alinishangaza mwishoni mwa mwaka jana wakati Gates Mgenge alipofanya interview ya wasanii sita na producer wawili kwa pamoja, interview ambayo ilikua ya kufunga mwaka kwani ilifanyika siku ya mwisho ya mwaka. Shyman ainishanga na kwamba alipiga simu hewani na aliweza kuimba wimbo ya kila msanii aliyekuwepo studio.
Dogo Richie pia ameweka wazi kanuni za label hiyo na kuweka wazi vigezo vya yeyote anayehitaji kujiunga.
Bonyeza Hapa Kumskiliza Dogo Richie

Comments

Popular posts from this blog

ThrowBackTrack.... MACHUNGU - Daddy Sele