Hii ndio Sababu Iliyowafanya Wasojali Band na Kelechi Africana kuiga wimbo wa Hello ya Diamond Platnumz
Watu wengi wametoa waoni yao kuhusu wimbo wa Nitalia Nawe wa Wasojali Band na Kelechi Africana, haswaa baada ya kuachiwa kwa video ya wimbo huo. Japo kua watu wameipa shavu video hio kwa jinsi ilivyoandaliwa na kusema iko kiwango cha juu zaidi na tofauti na video zingine walizotangulia kufanya Wasojali Band wengi wameonekana kukemea wimbo huo wakisema ya kwamba wamecopy beat ya wimbo wa Hello wa Diamond Platnumz.
Nilimtafuta manager wa Kubwa Entertainment, Athman Baba aka Babaz ambaye ndiye anayesimamia Wasojali Band na Kelechi Africana kumfikishia malalamishi hayo ya mashabiki na kujua ilikuaje wakaamua kutumia beat ya wimbo mwengine wakati Producer Noizer aliyetayarisha Nitalia Nawe anauwezo mkubwa na ubunifu wa hali ya juu na hashindwi kutengeneza kitu halisi.
Athman Baba alisema ya kwamba mwanzo kabisa angependa kidole cha lawama kisielekezwe kwa Producer Noizer kwani maelekezo yote ya project hio yalitoka kwake... Babaz alisema ya kwamba aliposikia wimbo wa Diamond-Hello aliupenda sana kiasi cha kua alikua anamaliza siku nzima ikiwa ndio wimbo pekee anaousikiliza.
"Beat ya Hello na hisia katika wimbo ule zake zilinigusa sana ndio nikaamua niwapeleke vijana wangu (Wasojali Band na Kelechi Africana) studio wafanye kitu kama kile. Sikutaka Noizer a,sample ile beat kwa kua angeongeza vitu vyake na ingepoteza ladha halisi ya kitu nilichokua nimependa. Kwa hivyo nikamwambia Noizer aigize ile kila kitu kilichopo ndani ya ile beat na kuna sauti flani zenye hisia katika Hello pia nikawaambia wajitahidi waziweke. Yote Tisa, Kumi ni kua nimetokea kuipenda Nitalia Nawe zaidi ya Hello kwa sababu mistari ni utunzi halisi wa Wasojali na Kelechi na beat niliyoipenda haijabadilika hata kidogo so kwangu mimi ni wimbo perfect sana."

Comments
Post a Comment