Hiki Ndicho Kitakachokua Kinatokea Kila Alhamisi Hapa Mombasa

Wasanii wengi hapa mkoani wamekua wakitamani sana angalau kama wana,launch video zao basi iwe launch kubwa, angalau ihudhuriwe na washikadai wengi wa mziki sana sana mashabiki na wasanii wenzao angalau kuwapa support. Imekua kitu kigumu kufanyika kwani hata kuna wakati Gates Mgenge alikua akifanya hivyo mbeleni katika event iliyokua ikiitwa Showbiz Wednesday lakini baadae ikasitishwa.
Kumekua na pilkapilka nyingi watu wakitamani wapate tena plartform ya pamoja ambayo watakua wakifanya uzinduzi kama sehemu zengine, mfano Nairobi wanavyofanya. Hatimaye plartform imetengeneza.
Kuanzia Alhamisi hii na kila Alhamisi inayofuata wasanii watakua wanaachia video zao mpya katika ukumbi wa Dans Lounge-Valencia Inn Mombasa. DJ Lenium atakua aki,host event hio na kila wiki kutakua na Dj tofauti watakao kua wanatumbuiza. Alafu kutakua na redcarpet ambapo watu watakua wanapiga picha kwa hisani ya Explode Africa Photography. Johnny Skani na crew yake ya Pungwe, Pwani Tv pia watakuwepo kila wiki pamoja na PiliPili Fm.
Alhamisi hii VIDEO NNE zitakua zinazinduliwa. PDay atakua anazindua DEAR MAMA aliyomshirikisha MCA mtarajiwa Cannibal. Vilevile Cannibal atakua anazindua video ya MDUDE. Kavalier atakua anazindua rasmi video ya MEMSODZA. Naye Dee Bouwy atakua anazindua NIPE aliyomshirikisha Chapatizzo.
Dj Rahj na DJ Geeps watakua waatusha burudani la kufa mtu wangu. Mashabiki, wasanii na washika dau wote wa mziki wanakaribishwa kuja kusherehekea na kuwapa support wasaanii wetu wanyumbani.
#CoastShowbiz254

Comments

Popular posts from this blog

ThrowBackTrack.... MACHUNGU - Daddy Sele