Shaa Biggy Anatamani Kufanya Collabo na Kigoto, Alafu ana Maoni Kuhusu Producer Totti

Msanii Sha Biggy kutoka hapa pwani amefunguka na kusema ya kwamba ako tayari kufanya kazi na msanii Kigoto. Akizungumza wakati wa mahojiano katika kipindi cha Kaya Flavaz ndani ya Radio Kaya na Sis Shannie,  Sha Biggy, amesema anakubali kipaji cha msanii Kigoto Mbonde na anaamini wanaweza kutoa kazi nzuri sana endapo watashirikiana watoe wimbo wa pamoja.
Akiongea na Shaniez, Shaa Biggy alisema..  “Kigoto ni miongoni mwa wasanii kutoka kanda ya pwani ninao wakubali zaidi na siwezi kataa nafasi ya kufanya kazi naye”.
Shaa Biggy pia alisema haoni ubaya Producer Totti kujitosa katika usanii kwani anaamini iwapo produce anaamini anaweza kuvuna zaidi katika usanii basi hatua yake haina makosa. Vilevile amemsifu Produce Totti kujitosa mzimamzima katika ulingo wa usani na kuwapa wasanii ushindani mkubwa

Comments

  1. Totti alipoanza kutoa miziki yake pia kama msanii hapo ndio alikuja kusahau clients wake. Kwa sasa sijafika studuoni mwake kumaliza songs zangu coz hana time ya kutuskiza , he never pick my calls , but production must go on.I hope one day he will pick my calls

    ReplyDelete

Post a Comment

Popular posts from this blog

ThrowBackTrack.... MACHUNGU - Daddy Sele