Sisi Wanasiasa ni Wanafik Sana, Asema Mike Sonko... Kunani Kwani?


Siku zote, wengi husema kwamba siasa ni mchezo mchafu. Na katika siasa hakuna adui au rafiki wa milele kwani vile vitu ambavyo wanasiasa hufanya mbele ya umma sivyo wanavyovifanya nyuma ya pazia... Yani siasa ni kama sanaa vile, ile uigizaji mwingi na mambo  mengi yanayofanywa na wanasiasa hua ni kwa maslahi yao tu tena kwa mda.
Hivi leo kupitia ukurasa wake wa facebook, Seneta wa Kaunti ya Nairobi, Mike Mbuvi Sonko amepost picha akiwa kinyozi akiwa pamoja Seneta wa Kaunti ya Mombasa Hassan Omar na Gavana, Ali Hassan Joho ambaye wengi wanajua ni adui yake mkubwa haswa kuanzi mwishoni mwa mwaka pale Rais Kenyatta alipokuja Mombasa bila kumtaarifu Gavana Joho. Sonko na Joho hurushiana maneno makali mbele ya umma hata nurusa siku moja wazichape ( Tazama Hapa).  Mombasa, Hassan Omar. Sonko aliambatanisha picha hiyo na maneno:
" Sisi politicians ni wanafik sana we are fighting in public but jioni tuko pamoja, we talk together. Wakenya wapendwa musikubali kupiganishwa tena na sisi. Pendaneni licha ya tofauti zenu za kisiasa. Siasa ni kama mawingu ya mvua yanapita ikinyesha so siasa itapita but Kenyans will remain where they are as brothers and sisters".

Hivyo basi wewe kama mwannchi wa kamaida unapoona wanasiasa wakifanya maigizo yao mbele ya umma, jua wapo kazini, watatukanana lakini mwisho wa siku wanakula sahani moja.

Comments

Popular posts from this blog

ThrowBackTrack.... MACHUNGU - Daddy Sele