Ushabiki au Unafiki?
Kila msanii hufanya kazi kwa bidii na kuhakikisha ya kwamba
anafanya kazi nzuri ya kuridhisha mashabiki wake na kukonga nyoyo za kila mmoja
atakayesikiliza kazi zake. Msanii hupata furaha pale anapokua na mashabiki sugu
ambao wanafagilia kazi zake kiasi cha kua wanaweza kumsaidia kumpigia debe kazi zake na kusimama kidete nayeye.
Hawa mashabiki sugu ndio wale ambao msanii akiacha kazi na
itokee wengine waikashif kazi ile au kuiponda basi hao watakua mstari wa mbele
kueleze uzuri wa kazi ile na kjaribu kufunika au kutetea kasoro zinazokosewa.
Jinsi shabiki anavyotetea kazi ya msanii na kumpigia debe huenda kukamjengea au
kumharibia msanii anayeshabikiwa. Kuna mashabiki ambao watajaribu kueleza mtu
anayeponda au kukashif kazi ya mtu ya kwamba aangalie ubora wa kazi na yale mapungufu
ayapuuze na kuna wale mashabiki ambao ukikosoa tu kazi ya msanii
wanayemshabikia basi ni matusi kwenda mbele. Hivi shabiki akimtusi mtu
anayekosoa kazi ya msanii, anamjenga au ana m,bomoa? Kwasababu endapo mtu
atatusiwa na mtu anayetetea kazi ya msanii basi huenda akachukulia ya kwamba Yule
mtu ametumwa au kibaraka wa msanii muhusika.
Mfano, Wasojali Band na Kelechi walipoachia video ya NITALIA NAWE, wapo waliokosoa jinsi walivyokopi Hello ya Diamond. Kwa shutma hizo, manager wao Alijitokeza na kusema ya kwamba kukopi Hello ilikua idea yake yeye kwakua alipenda sana wimbo ule wa Diamond. Mmoja ambaye hakupenda kukopi kule ilikua ni mtangazaji wa Kaya FM, Sis Shaniez aka Anti Virus, ambaye huendesha kipindi cha Kaya Flevaz, alisema ya kwamba kwa mwendo huu ndio maana utaweza kuona ya kwamba watu kama Koffi Olomide wanasema hawajui mziki au wasanii wa Kenya kwa sababu tumekosa uhalisia. Kukatokea Shabiki akamtusi Sis Shaniez kwa kua ametoa maoni yake na kusema ya kwamba watu kama hao ndio wanabania vipaji kwa kuonea wivu Wasojali Band na Kelechi. Haikuishia hapo, ‘shabiki’ Yule aliendelea kudai ya kwamba Shaniez alikosoa wimbo ule kwa kua alimtaka Manager wa Wasajali lakini akakataliwa…. Patamu hapo! Ikabidi niingie nyuma ya pazia kufuatilia.

Nilipomfutilia jamaa katika mtando akani,block. Ikabidi basi
nimfuate manager wa Wasojali, Athman Babaz nimuulize vizuri kuhusu Yule jamaa.
Babaz akasema ya kwamba aliona majibizano yale na alimfuata Yule jamaa katka
inbox yake lakini aliambulia matusi. “Yule jamaa m simjui, na hata ukiangalia
account yake haikai halisi nashangaa ushabiki wake. Kama kweli ni shabiki
asingekua anafanya vitu kama vile vya kutusi watu na kusema mambo ya uongo na
kutaja jina langu. Kusema kweli ni kitu ambacho sijaweza kukifurahia na
natamani hata ningejua ni nani”
Ushabiki kama huu ndio tunaweza uitaje sasa, kama itafikia point
shabiki aaanze kuharibu uhusiano wa manager wa msanii, msanii na presenter,
itakua ana mjenga au kumharibie msanii? Ushabiki kama hu n Ushabiki wa Kweli au
ni Unafik?
Comments
Post a Comment