Dalili Za Collabo Ya Nyota Ndogo, Ali B Na Susumila
Ndio vigogo wa mziki wa kizazi kipya hapa Pwani. Wamekua wakikonga nyoyo za wengi kwa tungo zao kwa mda wa miaka mingi sana. Wamekua wakiipeperusha bendera ya ZIKI LA NAZI, si Kenya tu bali Afrika Mashariki na dunia nzima kwa ujumla.
Kabla ya Nyota Ndogo kusafiri kuenda Tour nchini Denmark alikua anafanya projects zake Tempoz Records kwa producer AMZ. Tempoz pia ndio studio ambayo Susumila amekua akifanyia nyimbo zake nyingi katika siku za hivi karibuni. Na pia Ali B kazi yake ya mwisho, BEMBEA aliifanyia Tempoz na kunazo ambazo ziko jikoni anazifanyia Tempoz bado.
Watatu hawa wamejuana kwa mda mrefu kwani wamewahi kufanya kazi nyingi kwa pamoja kama vile roadshows, clubshows na hata show za kampeni za siasa ila katika hivi siku za karibuni wamekua na ukaribu sana kwani mara nyingi wamekua wakionekana pamoja katika mikahawa, tamashani na hata studio..haswaa TEMPOZ.
Kwa kua wamekua wakipatana mara nyingi Tempoz, inakisiwa ya kwamba watatu hawa wanatayarisha wimbo wao wa pamoja. Haijaweza kubainika kabisa iwapo ni colllabo wanaanda au ni urafiki wao ndio umezidi kujengeka kwa kua wanapatana mara nyingi kwa pamoja ila kupatana kwao studio kunachochea sana hizi tetesi za collabo ya watatu hao. Ni mda tu, na ukweli utabainika.

Comments
Post a Comment