Nyota Ndogo Aweka Wazi Siri Zinazomfanya Adumu Katika Mziki


Nyota Ndogo ni mmoja kati ya wasanii ambao wamedumu katika mziki kwa kipindi cha mda mrefu na hadi leo bado jamii inamtambua na heshima yake bado iko palepale. Ni msanii ambaye anaweza kukaa kwa mda wa hata wa miaka bila kutoa wimbo na bado anapiga shows za maana.
Hivi mbona kuna wasanii wengi wanakuja wanapotea wanamuacha huyu mwanadada palepale? Hivi mbona wasanii wengi wanatoa hits kila siku ila hawafikii heshima ya Nyota ambaye ni mkongwe na hadi leo heshima yake inazidi kupanda?
 Nikimnukuu Nyota, ..."Mimi kama Nyota Ndogo nimetunza heshima yangu kama mama na nimekua kwenye hii industry kwa miaka 16 kwa hivyo ninaweza kupata shows sio kwa sababu niko na kitu kipya hewani bali ni kwa sababu ya heshima yangu na pia niko na nyimbo zinazodumu hewani"....
Haya hapa ni mahojiano ya Nyota Ndogo na Kelvin Jilani( MtuBei) ambayo nahisi kuwa yana siri nyingi saana za mafanikio na kudumu katika mziki....
Bonyeza HAPA kuskiliza mahojiano hayo.

Comments

Popular posts from this blog

ThrowBackTrack.... MACHUNGU - Daddy Sele