Susumila Aongelea Swala la Ajira Na Vijana Wa Pwani Kuhusishwa na Uvivu.


Kulingana na msanii Susumula ni kwamba changamoto za ukosefu wa kazi ziko katika kila upande wa Kenya na sio pwani pekee. Susumila amefunguka na kusema kuwa uvivu uko kila mahali Kenya hii ila kitu kinachofanya mpaka pwani inahusishwa na uvivu ni kwa sababu ni mahali ambapo pako kwenye macho ya wengi tofauti na sehemu zingine za Kenya.....

"ukiangalia barabarani utaona vijana wamekaa wamevaa jezi za kwamba wanataka kupeana squad kwa matatu tayari ile inaonyesha moyo wa kuwa wanataka kufanya kazi".
Kwa upande wa suluhisho la shida hii, msanii huyu ambaye anatarajiwa kuachia video yake na Kaka Sungura wiki ijayo amesema kuwa ni vizuri vijana wazingatie elimu maana unapokua na elimu hata kama huna kazi utakua na ujanja ujanja wa maisha.

Susumila ameomba watu wawekeze kwenye talanta za wapendwa wao maana talanta ni moja kati ya ajira kubwa saana Duniani.
Bonyeza HAPA kumskiliza Susumila aka Nugu akifunguka katika mahojiano na Kelvin Jilani(Mtu Bei)

Comments

Popular posts from this blog

ThrowBackTrack.... MACHUNGU - Daddy Sele