Tamasha Kubwa Afrika Mashariki Kufanywa Mombasa Wikendi Hii



Mwishoni mwa mwezi huu, Siku ya Jumamosi 30 Aprili, Mombasa itakua mwenyeji wa takriban wamama 100,000 kutoka sehemu mbalimbali hapa afrika mashariki. Wanawake hao watakua wanahudhuria uzinduzi rasmi wa mradi wa AMSHA MAMA. 


AMSHA MAMA ni mradi wa kuwasaidi ake na mama kujiendeleza na kuwapa uwezo wa kujitegemea kibiashara na kujiinua kimaisha. Mradi huo unaendeshwa na Joe Kariuki ambae alikua mmiliki wa recording label ya CANDY N CANDY na ambaye hivi majuzi aliorodheshwa kua mwamfrika nambari mbili mwenye maono makubwa, katika orodha ambayo aliwashinda wangwiji kama vile bilionea Aliko Dangote

Katika uzinduzi huo, kutakua na maonyesho ya biashara mbalimbali kutoka kwa wamama kutoka pande zote za afrika mashariki, wakiuza na kuonyesha baadhi ya biashara na bidhaa zinazowaendesha maisha yao. Tamasha hio kubwa ya uzinduzi wa AMSHA MAMA utafanyika katika uwanja wa mama ngina na kutakua na burudani la kukata na shoka kwani kutakuwepo na Susumila, Sudiboy, Nyota Ndogo, Ali B, DJ Digoh, Shaniqwa, MC Chris na Mc Gates Mgenge na KIINGILIO itakua BURE NA WAZI KWA WATU WOTE.

Comments

Popular posts from this blog

ThrowBackTrack.... MACHUNGU - Daddy Sele