Ali B Aeleza Siri Inayomfanya Kupata Dili Za Tamasha Kubwa Za Kitaifa
Bila kupinga, Ali B ndiye msanii wa mziki wa kizazi kipya kutoka Pwani ambaye amewahi kutumbuiza katika tamasha nyingi za kitaifa kuliko msanii yeyote. Mbona yeye? Siri ni nini?
Msanii Ali B amesema kua heshima ndio kiini kikubwa kinachomfanya anawakilisha na kukubalika na kila rika. Kulingana na Ali B ni kwamba heshima yake imemjengea brand kubwa kufikia kiwango cha kupewa heshima na fursa ya kuweza kutumbuiza katika sherehe mbalimbali kubwa za kitaifa kama vile Jamuhuri Day na Madaraka day hadi kwa hafla zinazofanyika hadi ikulu.
Bila shaka hii ni ndoto ya kila msanii kuweza kufikia viwango hivi katika malengo yake ya kimuziki hivyo basi kufanikiwa kwa Ali B katika swala hili lazima kuwe kuna siri fulani anayoitumia.....
"usanii sio kuimba tu bali ni hadi vile unavyojiweka kwamba je unaweza ukatumbuiza mbele ya mawaziri au mbele ya rais?kwa sababu usiwe umetobolewa maskio umejichorachora mwili mzima alafu wataka kusimama mbele kumtumbuiza ruto na uhuru,so tusiangalie tu sanaa,pia tujiangalie je naweza kusimama na mtu fulani?"
Pia kupitia kauli yake, Ali B amesema kuwa yeye kama msanii mkubwa kuzidi kupata shows kubwa sio kupendelewa bali ni kwa sababu yeye amejua kuji package na kujenga brand kwa kipindi cha mda mrefu pamoja kuwa na mtindo unaoweza kumtambulisha kiurahisi....
"show kubwa ninapozipata mimi pengine ni kwa sababu kazi yangu ni nzuri, kitu ni kwamba mimi nawapa ushauri mmoja, originality ni kitu muhimu saana wasanii wengi saa hii wanawaiga kina diamond wengine wanawaiga kina Davido hadi hakuna mtindo unaowatambulisha,ukiiga msanii flani inamaanisha msanii huyo unayemuiga akifeli basi wewe pia utafeli tu"
Kwa sasa Ali B anajiandaa kuachilia video ya wimbo wake kwa jina "NZELE" ambayo inatoka wiki moja ijayo.
Bonyeza HAPA au HAPA kumsikiliza Ali B akifunguka
Comments
Post a Comment