Dazla-Simuigi Diamond, Labda Yeye Ndio Ananiiga Mimi


Msanii hit maker wa track ya KIDE KIDE, Dazla Kiduche amekana madai ambayo yameenea mtaani kuwa anamuigiza Diamond Platinumz. Akiongea katika kipindi cha MwakeMwake cha Pilipili FM na Gates Mgenge, Dazlah ameweka wazi kuwa yeye anajiweka yeye kama yeye na endapo kuna kufanana kwa mitindo na mienendo basi iwe labda Diamond ndio anamuigiza yeye.
Dazlah aliyaongea haya wakati akitambulisha kichwa kipya kutoka Tee Hits, Cashhomey ambaye alikua akitambulisha ngoma yake kwa jina Yelele.

Kwa sasa Dazlah anajitayarisha kuanza kutayarisha video wiki ijayo ya wimbo wa Kitoriro, kolabo aliyoshirikishwa na mwenzake kutoka Tee Hits, Wynas.

Comments

Popular posts from this blog

ThrowBackTrack.... MACHUNGU - Daddy Sele