Ziki La Nazi Haikua Idea Yangu Lakini Tutumie Kama Identity Ya Mziki Wa Pwani, sistiz ALI B


Kwa kipindi cha mda mrefu saana wasanii pamoja na wadau wa mziki wa pwani ya kenya wametafuta sana jina ambalo litakua nembo itakayobeba utambulisho wa mziki wa pwani. Mziki wa maeneo mengi umepata majina maalum kuutambulisha kwa mfano Nairobi kuna mziki mtindo wa Genge, Ghipuka, Kapuka huku Tanzania wakijivunia kutambulika na jina la Bongo Fleva

Harakati za kuja na jina maalum litakalotambulisha mziki wa pwani ya kenya zimeonekana kuchipuka na kwa sasa kuna jina ambalo baadhi ya wasanii wameanza kulikumbatia. Msanii Ali B kwa kipindi cha mda sasa ameskika akitumia nembo ya "ZIKI LA NAZI" kwenye nyimbo zake huku akifikia kiwango cha kutoa wimbo uliobeba jina hilo.Ni nembo ambayo kufikia sasa wasanii kadhaa wameanza kuitumia na imeanza kukita mizizi. 
Swali je nembo hii ilitokea wapi? Kulingana na Ali B sio yeye aliyebuni nembo hii.......

"kusema kweli ziki la nazi tulikua tunazungumzia kuhusu jina litakalowakilisha mziki wetu,sasa katika meeting yetu wasanii pale Big Tree kila mtu alitoa wazo lake, ilipofika zamu ya Producer NJE akasema kuwa mziki wetu uitwe ziki la nazi alivyosema hivyo mimi nikasema huu msemo wa Producer NJE nimeukubali, sasa pale wasanii wengi walikataa wengine kidogo wakakubali sasa mimi pale nikaukubali na nikaamua kwamba hili jina nitaliuza ndio maana sasa kila mziki nitakaoutoa nataja ziki la nazi hadi sasa watu wameanza kuukubali. Sasa kila mtu anajua kuwa mimi ndio nimejibrand kama ziki la nazi lakini ziki la nazi ni wazo lilikuja na Producer NJE mimi ndio nikalibeba kama brand".

Ali B amesema kuwa juzi kati katika party ya Nyota Ndogo , Pweza Party walikua na kikao kama wasanii ili kuhimiza wasanii kuliuza jina hili ili liwe kama nembo ya mziki wa pwani.
JE WEWE KAMA SHABIKI WAZO LAKO NI LIPI KUHUSU JINA HILI?

Comments

Popular posts from this blog

ThrowBackTrack.... MACHUNGU - Daddy Sele