Dogo Richy Awajibu Wanaoiponda Yoyoba Remix
Msanii Dogo Ree tokea juzi amekua akigonga vichwa vya habari baada ya kuachilia video ya Yoyobah Remix aliyomshirikisha Calvo Mistari. Baada tu ya Richie kuachilia video hiyo baadhi ya washikadau pamoja na mashabiki wa mziki walivamia mtandao na kuiponda video hiyo huku wengi wakidai kuwa ni mbovu na haijaipiku Yoyoba original.
Baada ya mitazamo kibao kuanikwa kwenye mitandao, Richie amefunguka na kuweka wazi kuwa anaheshima maoni ya kila mtu.....
"Mimi ninaheshimu maoni ya kila mtu ila wangeisifu yoyobah original kiwango cha vile wanavyoiponda remix then ningefika mbali saana,alafu mimi ningewasihi watu kuwa hakujaharibika kitu sababu kama remix haujaipenda original ipo unaweza ipa shavu"
Huyu hapa Dogo Richie msikilize ujue anaowatupia lawama pamoja na
mtazamo wake kuhusu remix hiyo...Je yeye mwenyewe ameikubali ameikubali?
Bonyeza HAPA
Bonyeza HAPA
Amazing
ReplyDelete