Gates Mgenge Aongelea Kuhusu Kuhongwa Na Wasanii
Mtangazaji maarufu wa kituo cha PiliPili Fm, Gates Mgenge amejitenga na lawama ambazo kwa kipindi cha mda mrefu zimemuandama kuwa amekuwa akipendelea wasanii flani katika kipindi chake. Kulingana na Gates ni kwamba hawezi kamwe kumpendelea wala kubana mziki wa msanii yoyote.
"cha msingi na sekondari mi kazi huingia saa tano mpaka saa moja na huwa napata kila kitu kishapangwa mziki ushapangwa na nikaambiwa link zangu ni ngapi so cha msingi kwangu ni sauti na creativity yangu lakini maswala ya mziki gani nitakaocheza hapo ni pagumu maana hiyo ni kazi ya ma producer wangu"......
Gates ambaye pia ni MC maarufu katika mkoa wa pwani pia amekana madai kuwa huwa yeye amependelea wasanii flani katika shows zinazoandaliwa huku akisema kuwa hajawahi husika kabisa kwenye kuchagua wasanii kutumbuiza kwenye shows. Huyu hapa Gates Mgenge, akieleza vigezo halisi vinavyohitajika ili mziki wa msanii upitishwe na ma producer wa show yake pamoja na siri ya kutawala shows za pwani.
Bonyeza HAPA
Waambie waache zao zakishamba na wamuache Gets atambe
ReplyDeleteWaambie waache zao zakishamba na wamuache Gets atambe
ReplyDelete