Huenda Producer Tee Akatiwa Mbaroni
Mwaka wa 2013, studio aliyokua akifanyia kazi Producer Tee, Da'Face Music ilivamiwa na vifaa vyote vikaibiwa. Aliyekua akimiliki studio hio ni Zakumera Zaky. Kwa kua Tee ndiye aliyekua amekabidhiwa vifaa hivyo ilibidi waingie katika makubaliano na Zakumera ya kwamba Tee ndiye atakayelipa hasara hio ya vifaa vilivyoibiwa.
Kulingana na mdokezi wetu ni kwamba vifaa vilivyokua vimeibiwa vilikua na thamani ya zaidi ya kshs.400,000 lakini wakaamua kushukisha thamani na kumpa wepesi Tee kwa kumuambie alipe kshs.252,000. Katika makubaliano yao, ambayo nilifanikiwa kuona copy yake ni kwamba walikubaliana ya kwmba Tee alikua atalipa kshs. 10,000 kila mwezi.
Kulingana na mdokezi wetu, toka Tee na Zakumera waingie katika makubaliano hayo mwaka wa 2013, Producer Tee amelipa kshs. 26,000 jambo ambalo limemgadhabisha Zakumera. Siku ya Jumatano, Producer Tee aliitwa katika kituo cha polisi cha Bamburi na kupewa amri ya kwamba alipe deni hilo alilonalo kufikia Ijumaa, na kiasi atakacholipa kisiwe chini ya kshs.100,000 laa sivyo atatiwa mbaroni na kupelekwa kortini.
Ni amri ambayo imemtia tumbo joto kwani kulingana na mdokezi, ni kwamba Tee amejaribu kumfikia Zakumera kwa njia ya simu angalau akubali kiwango atakachoweza kupata ifikapo siku ya Ijumaa lakini zuhudi hizo za kuwasiliana na Zakumera zimegonga mwamba.

Dah ishakua shida
ReplyDelete