Je, Chapatizo Ameacha Mziki?
Track yake ya mwisho kuachia ilikua mwanzo mwa mwaka huu, ni track ambayo aliachia kimyakimya sana hata wapo wengi hawana habari ya kua aliachia wimbo kwa jina VIGUDIGUDI. Pengine ilikua ndio ishara ya kwamba amechoshwa na pandashuka za mziki ndio maana akaiachia tu hivihivi, tofauti kabisa na wimbo alioshirikishwa na Dee Bouwy-NIPE.
Kando na kuonyesha kutokua na msukumo na kazi yake ya mziki, Chapatizo ameonyesha kujituma sana katika u,MC, uchekeshaji na hivi karibuni uigizaji. Ni ishara ambazo zimeweza kuzua minong'ono ya kwamba Chapatizo huenda akwa ameacha mziki na kujitosa katika kazi hizo zingine ambazo zimeonyesha kumkubali kwa haraka na kumfanya aendelee kuishi vizuri.
''Uingiziaji na uchekeshaji nilianza toka 2014 ila ilikua ni filamu fupifupi za comedy lakini kwa sasa nimefanya filamu moja kubwa na Ashiner Pictures, watayararishaji wa kipindi cha Almasi. Tumemaliza ku,shoot filamu moja na ya pili tutaanza hivi karibuni. Ni filamu ambayo siwezi iongelea kwa sana kwa sababu mkataba wangu hauniruhusu ila waandalizi wakiwa tayari wataachia details kuhusu filamu hio.
Kuhusu mziki, kwa sana niko kimya kwa mda, ila si kwamba nimeacha mziki lakini niko katika hali ya kutayarisha kazi zangu mpya. Kuna kazi nazifanya na nitarudi tofauti kabisa, si vile watu walivyonizoea. Naji,brand na kuji,package kitofauti...watu wataelewa vizuri wakati nitakapo anza kuachia kazi zangu mpya.'' Chapatizo ameeleza katika mahojiano na meza yetu ya habari.
Comments
Post a Comment