Kibibi Salim Aongelea Uigizaji Na ndoa Yake
Msanii wa filamu Kibibi Salim anayebeba uhusika wa ''chiriku'' kwenye tamthilia ya Almasi amefunguka na kuwahakikishia wote walio na ndoto ya kuingia katika tasnia ya uigizaji kuwa tasnia hiyo ya uigizaji iko na hela ila kinachohitajika ni talanta, bidii na subira.
''ukiona nimetulia silalamiki kwenye hii sanaa ya uigizaji jua naridhika na ninachokipata. Sanaa ya uigizaji inalipa, nime,settle hapo kwa sababu inalipa hata kama atfiirst haitakulipa inavyotaka ila mtu huanzia chini..'' Kibibi ameeleza.
Kibibi ambaye pia ni mke wa ndoa wa msanii Susumila amesema kuwa yuko mbioni kupitia msaada wa mumewe kufungua studio yake itakayoshuhulika na utayarishaji wa filamu miaka miwili ijayo.
Mbali na mipango yake kwenye uigizaji, Kibibi pia amefunguka mengi na MtuBei kuhusu ndoa yake na msanii Susumila..kwa kina zaidi fuata link kumsikiliza Kibibi kwenye mahojiano na MtuBei HAPA
Comments
Post a Comment