Msanii Lil Mizze Kuhamisha Kambi Kutoka Malindi Hadi Mombasa
Msanii kutoka maliandi ambaye track yake iliyopo hewani kwa sasa ni SIJUI KWANINI amefunguka ya kwamba anahamisha kambi yake hadi mjini Mombasa.
Lil Mizze ambaye anatarajia kuachia video ya SIJUI KWANINI mapema mwezi ujao amesema ya kwamba anapata ugumu kufanya mziki akiwa mjini Malindi. Mizze anasema changamoto anazozipata kwa sana zinasababishwa na yeye kua mjini Malinidi hivyo basi kuja Mombasa kutampa wepesi wa kazi yake ya mziki.
'Vitu vingi ninavyovihitaji ili kufanikisha mziki wangu vipo Mombasa, kama vile studio, vituo vya habari, ma,dj...so naona itakua vyema nikijisongeza karibu na resources hizi ili niweze kufanikisha safari hii yangu ya mziki." Lil Mizze amefunguka.
Comments
Post a Comment