Msanii Wa BongoFleva Kuja Mombasa Kufuata Huduma Za Producer Amz



Msanii wa bongo fleva kwa jina Rich One ambaye alifanya vizuri saana na ngoma hatuna kitu aliyomshirikisha juma nature,ameelezea matamanio yake ya kusafiri hadi kenya kuutafuta mkono wa producer wa mombasa Amz Wa Leo ikiwa nia muhimu ni kutayarishiwa bonge moja la project.
Kulingana na Rich One ni kwamba ameamua kufunga safari hiyo kufuata huduma za Amz baada ya kuskia mdundo wa ngoma ya Cannibal na Juma Nature ambayo ilimdatisha saana kwa sababu ya utofauti wake.
"Naja na Nature tuje tugonge bonge la ngoma na Nature, nimeskia ile ngoma ya Cannibal na Nature amepiga beat kali saana"......Rich One anapania kufanya project hiyo na mkongwe Juma Nature na huenda wakafika mombasa mda wa kama wiki mbili zijazo.

Comments

Popular posts from this blog

ThrowBackTrack.... MACHUNGU - Daddy Sele