Msanii Wa Kike Kutoka Mombasa Aliyejibu Wimbo Wa Alikiba-AJE



Grace Mueni ndio jina lake la serikali, ila katika anga za muziki anajulikana kama Ngunash. Ni msanii chipuka ambaye ameanza kupata kile ambacho wasanii wengi chipuka hukipigania-Aiplay. Hii ni baada ya kuachia track kwa jina NAJA.
Ni track yake ya kwanza kuachia rasmi. Japo alishawahi ku,record track mbili, moja na producer TK2 na nyengine na Producer Triple A/ Mo Town Reords hajawahi kuziachia kwani ni juzijuzi tu ndio alisajiliwa na Mtwapa Records ambayo iko chini ya uangalizi wa Producer Mswazi Mayuro na mkataba wao hauruhusu ngoma hizo za mbeleni kuachiwa.

'niliposkia AJE ya Alikiba nilihisi kana kwamba alikua ananiimbia mimi, ndio nikapata mskuma ya kujibu wimbo ule na kutengeneza track hii''... Ngunash amenieleza. Ni track ambayo ameijibu kw ubunifu na ameonyesha uwezo wake wa sauti na Producer wake, Mswazi Mayuro ameitendea haki track hii.
Download / Listen HERE or HERE

Comments

Popular posts from this blog

ThrowBackTrack.... MACHUNGU - Daddy Sele