Rikky Bekko Ataja Vigezo Vya Kutoboa Kimataifa

Mtayarishaji wa video za mziki anayefanya vizuri kwa sasa Ricky Becko amewahimiza wasanii kuwekeza vilivyo katika kazi zao ili kuongeza thamani ya bidhaa wanayoingiza kwenye soko la muziki. Kulingana na Becko ni kwamba njia pekee ya kupenya kwenye ramani ya mziki wa kimataifa ni kutoa kazi ambazo zitakua na ushindani mkubwa katika soko la sasa la mziki ambalo limezidi kuwa gumu kila kukicha.
Becko amesema kuwa wasanii wengi wanatosheka na mafanikio madogo na wanakosa malengo makubwa katika kazi wanayoifanya.  

"I think wasanii wengi wako kwa comfort zone... they are comfortable with what they have achieved like. Kuna watu wameingia kwenye mziki kwa sababu ya kupata fame, wengine kupata madame so mtu akiwa famous akipata tudem tunamuita ita pale basi ametoshek''


Becko amesema ili msanii kufanya kazi na yeye kwanza lazma msanii awe na talanta, pili lazima wimbo wenyewe lazima uwe na ubora. "msanii akija na wimbo ambao hauko kwenye viwango vinavyostahili sitamfukuza ila nitamrefer kwa producer mzuri kwanza"
Huyu hapa Ricky Becko msikilize akiongea kuhusu vigezo vinavyohitajika ili kuchezwa MTV BASE, TRACE na Vituo vingine vya kimataifa.
Msikilize  HAPA

Comments

Popular posts from this blog

ThrowBackTrack.... MACHUNGU - Daddy Sele