Nyota Ndogo Atumiwa Katika Utapeli
Kila mtu ako mbioni kujitosheleza.... Wengi wako mbioni kutafuta pesa za kujikimu na wengine pia wako mbioni kutafuta mapenzi angalau roho zao zitulie wafarijike.
Katika kutafuta pesa, wapo wanaotafuta pesa kwa njia halali wengine haramu ili mradi tu mwisho wa siku pesa iingie mfukoni. Na wanaotafuta mapenzi nao vilevile wanatumia njia tofauti kupata watakacho.
Ukizingatia ya kwamba siku hizi mambo mengi yanafanywa mitandaoni, basi ni wazi kwamba utapata wengi wanapata pesa kupitia mitandao na wapo wanaopata wapenzi kupitia mitandao.
Uganda kuna ukurasa wa facebook ambao unadai kukutanisha wapenzi. Ukurasa huo umebandika picha ya Nyota Ndogo akiwa na bwanake na wakidai kwamba hao ndio waliwezesha na kufanikisha wawili hao kukutana hadi kuishia katika ndoa. Katika ukurasa huo wamedai ya kwamba Nyota Ndogo anaitwa Sarah na bwanake ambaye jina lake ni Neilsen amebandikwa jina la Raymond.
Juhudi za Nyota Ndogo za kufikia wenye ukurasa huo kupitia nambari za simu zilizowekwa ili kuwakanya na kuwaambia wakome kutapeli watu kutumia yeye zimegonga mwamba kwani simu zake hazishikwi.
Vilevile Nyota Ndogo anajitayarisha kuachia ngoma yake mpya kwa jina Subira Yangu baada ya kipindi hiki cha mwezi mtukufu wa Ramadhan. Subira Yangu ni track ambayo ni ya uhamasisho na inatarajiwa kuachiwa Julai 8.

Aya braza mablogger kuchocha ndio apa sasa
ReplyDeleteSawa
ReplyDelete