Producer Khalid Kuwashtaki Waandalizi Wa Tuzo Za Mombasa Awards 2016


Producer ambaye hafichi hisia zake kila wakati pale anapokerwa au kufurahishwa na jambo flani haswa katika tasnia ya burudani, Prodcuer Khalid ameandika barua wazi kwa waandalizi wa tuzo za Mombasa Awards 2016. Tuzo hizo zimevutia hisia mbalimbali baada ya kutangaza orodha ya nominnees kama vile wasanii wengine kutoa katika tuzo hizo, Odinare Bingwa akiwa mmoja wao na wengine kusema hawataki kuhusishwa na tuzo zozote.
Leo kupitia ukurasa wake wa facebook, Khalid amejitokeza na kuandika ujumbe huu akiuelekeza kwa maandaaji wa tuzo za Mombasa Awards huku akipendekeza sheria kutiliwa maana hata kwa maandaji wengine wa tuzo ili tuzo hizo ziweze kunufaisha wasanii si waandaaji wa tuzo tu....
To Whom it may concern,
‪#‎MOMBASA_AWARDS‬
kwa miaka mingi wasanii wa pwani wamekuwa wakibebwa kama magunia ilihali wenzao wa Nairobi au Bongo wakibebwa kama mayai.Tuzo nyingi zilizopita zimekuwa na tabia ya kuweka wasanii kwa list zao bila taarifa, ilihali mshindi ashajulikana. Wasanii hao hao ndio watapiga promo awards hizo kila mahali mpaka mashabiki wao waamue ku support event hiyo. Lakini haya yote huwa hayana manufaa kwani hata show wakiperform usiku huo hata shilingi hawapati, wala hakuna special recognition yoyote.

Najua huwa mwaandika proposals kwa makampuni kufadhili Tuzo zenu, lakini manufaa kwa wasanii wa pwani hakuna. Mtalipia ndege na hoteli wasanii wa Bongo na Nairobi, muwa treat kama VIPs na wenzao wa mombasa hamuwashughulikii. Hii ni wazi kuwa mmajifanyia Tuzo hizi kwa manufaa yenu wenyewe.
Ili kukomesha tabia hii nimeamua kuwapa #MOMBASA_AWARDS siku saba kurekebisha swala hili kwani hata nyinyi mumefuata mkumbo huo. Kwanza mumeweka majina ya wasanii bila kuwataarifu na kuanza marketing ya awards zenu. Hicho ni kinyume cha sheria za Kenya. Msanii anang'ang'ana sana kufika pale alipo. Haumufanyii favor yoyote kwa kumu nominate. Hilo ni jasho lake na mnafaa kuliheshimu.

Ili kukomesha tabia hii ni rahisi, wasanii wote waliowekwa kwenye list bila taarifa wataandikisha taarifa kwa lawyer wangu wakilalamika kutumika kwa majina yao kibiashara bila taarifa na maelewano. Na kila msanii atadai kulipwa kwa kutumika vibaya. Gharama za lawyer na mahakama nitazigharamia ilimradi hii tabia ikome. Na kabla kesi kuanza nitaomba mahakama isitishe Tuzo hizi na nyengine za kipuzi kama hizi indefinitely. 

Siku saba mnazo kuitisha mkutano Kwanza, kujijulisha nyinyi ni akina nani. Pili, mnamalengo gani na wasanii na Tuzo zenu. Tatu, wasanii watafaidika kivipi kwenye Tuzo hizo na baada ya Tuzo hizo. Na kwa nini mkaweka majina ya wasanii bila taarifa yao ambacho hicho ni kitendo cha kihuni. Na mumetumia criteria gani kuchagua wasanii, manake nimeona mumejiwekea tu wasanii kwenye list bila ujuzi, hekima na mwongozo dhabiti.

Wacheni niwakumbushe tena, hamumufanyii favor msanii yoyote kwa kumu nominate kwa hizo Tuzo zenu kwani ni jasho Lake na haki yake.Mko na siku saba kurekebisha hili, Lau sivyo tukutane mahakamani....

Comments

  1. Hapo Huyo kaka amenena ukweli kabisa , Coast kuna upumbavu mwingi sana Wa kudhulumu wasanii. I support Khalid on this and no body should ever miss use artistes again on our Kenya land.

    ReplyDelete
  2. Shukran sana ndugu yangu.. I support u mia kwa mia... Washatuzoea sana na kutumia vipaji vyetu kujiekea mihela mifukoni.. Round hii hawatoshi......

    ReplyDelete
  3. I support the guy he has a very strong point. Being nominated is not a favour it is through hard work, financial struggle and determination that has led you to a platform that they have recognised you. Nw that should b respected

    ReplyDelete
  4. I support the guy he has a very strong point. Being nominated is not a favour it is through hard work, financial struggle and determination that has led you to a platform that they have recognised you. Nw that should b respected

    ReplyDelete

Post a Comment

Popular posts from this blog

ThrowBackTrack.... MACHUNGU - Daddy Sele