''Rihaha The Boss'' Atangaza Kugombea Ubunge Kilifi North
Hashim Aida Omar ni mwanabiashara maarufu sana katika Kaunti ya Kilifi na Mombasa vilevile ila wengi wanamjua kwa jina la Rihaha The Boss, manager wa Susumila na pia juzi juzi aliwa,sign Guf Lyder, Kabambe, Dhilly Dhilly na Crash V. Ni mmiliki wa Rihaha Investments, kampuni ambayo inamiliki viwanda na kampuni kadhaa. Mwishoni mwa wiki jana, Rihaha alimfanyia bonge la harusi mmoja wa mfanyikazi wake kwa jina Khamisi.
Ni sherehe iliyofanyika Rihaha Farm, nyumbani kwa Rihaha, Mtondia, Kilifi. Ni sherehe ambayo ilihudhuriwa na watu mbali mbali wakiwemo wanasiasa, wanabiashara na wasanii wengi.
Katika sherehe hio, Rihaha alichukua fursa hio kutangaza ya kwamba amejitosa rasmi katika kinyang'anyiro cha 2017 na atakua ulingoli kumenyania ubunge katika eneo bunge la Kilifi North.
''wana Kilifi wajiandae kw amabadiliko kwani mambo nitakayoenda kuyafanya yatashangaza wengi... ni wakati wa Kilifi kuamka na kubadilika na maendseleo yafanyike...nitawajibika na kubadilisha hii Kilifi kwa kiasi kikubwa sana. Mimi kama mwanabiashara, najua wanaofanya biashara wanahitaji nini na wanachi wanahitaji nini ili maisha yawe rahisi, mepesi na bora kwao na hivyo basi siwezi kuwaangusha" Rihaha alisema akitangaza hatua hio anayoenda kuipiga.
Comments
Post a Comment