Uja Uzito Ndio Ulimnyamazisha Shiney Katika Mziki
Msanii kutoka studio za Big Foot, Shiney ambaye pia ni 'babymama' na pia mpenzi wa Producer Baindo amefunguka na kusema kuwa kimya chake katika mziki kimesababishwa pakubwa na ujauzito aliokua nao. Kulingana na Shiney ni kwamba baada ya kuachilia track ya Kidonda Cha Mapenzi, ratiba yake ilikua ni kutayarisha video tatu mfululizo ambazo mashabiki wake wamekua wakizililia lakini kabla ya kuanza project hizo baraka za ujauzito zikamfikia.
"Mimi sio msanii wa kwanza kujifungua kwa hivyo kujifungua kwangu hakutawahi kuathiri kabisa kazi yangu ya mziki.....Kuna ngoma ambayo nimefanya na Mr Bado ambayo nimeifanya saa hii
nasubiri kurudi sawa alafu kazi iendelee. Baada ya hapo ndio nitaanza
kushughulikia video ya Jicho maana hiyo ndio mashabiki wangu wana
demand"
Huyu hapa Shiney msikilize akizungumzia mziki wake, familia, mtoto pamoja na Baba mtoto...
Bonyeza HAPA
Huyu hapa Shiney msikilize akizungumzia mziki wake, familia, mtoto pamoja na Baba mtoto...
Bonyeza HAPA
Comments
Post a Comment