Wasojali Band Kuzindua Rasmi Wimbo Mpya Mjini Taveta

Kilele cha  burudani kwa shabiki kutoka kwa msanii ni pale msanii anapotumbuiza jukwaani.
Ukitaja wasanii tano bora wanaoteka nyoyo za wengi wanapokua jukwaani hapa mkoani, Wasojali Band hawawezi kukosa katika listi hio.  Hawa ni vijana ambao walichipuka tu mwaka jana ila wameweza kutia bidii sana katika sanaa kwa kuonyesha uwezo wao wa kuimba na kutumbuiza jukwaaani.

Hawa vijana hawana mchezo na performance zao kwani hua hawapigi show chini ya masaa matatu jukwaani. Si eti hua wanarukaruka tu juu chini na kuhangaika stejini ila hua wanacheza na style za mvuto na kuchangamsha si haba.
Kwa mara ya kwanza katika Kaunti ya Taita Taveta, Wasojali Band watakua wanafanya uzinduzi rasmi wa wimbo wao mpya wa AUMBORA, Club Tangu-Hotel Challa, Taveta katika show ambayo itakua na kiingilio cha Kshs.200 tu.

Comments

Popular posts from this blog

ThrowBackTrack.... MACHUNGU - Daddy Sele